Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass

Ugonjwa wa amiba au amoeba ni ugonjwa unaosababishwa na kimelea(parasite) kinachoitwa Entamoeba histolytica.

Ugonjwa wa Amiba (Amoebiasis) kwa kifupi

Amiba ni maambukizi yanayosababishwa na kimelea kinachoitwa Entamoeba histolytica. Huambukizwa kupitia chakula au maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye vimelea hivyo.

Entamoeba histolytica  ni kimelea kwenye kundi la anaerobic parasite na kwa mara ya kwanza hupatikana kwenye Utumbo mpana(colon);

Ingawa kutokana na Sababu zisizofahamika, kimelea hiki kina uwezo wa kutoka na kupita moja kwa moja mpaka kwenye Ini na kusababisha tatizo ambalo hujulikana kwa kitaalam kama amoebic liver abscesses."

Kimelea hiki kinaishi kwenye Utumbo wa binadamu na kinaweza kusababisha ugonjwa wa amoeba kwa mtu yeyote anayekula au kunywa kitu kilichoambukizwa na kimelea hiki.

Katika makala hii, tutajifunza kuhusu sababu, dalili na matibabu ya ugonjwa wa amoeba.

KUMBUKA; amoebiasis-Ndyo ugonjwa wenyewe ambao chanzo chake ni kimelea au parasite anayejulikana kama Entamoeba histolytica.

CHANZO CHA UGONJWA WA AMIBA

Hivo basi kama tulivyosema, chanzo cha ugonjwa wa amiba ni mashambulizi ya vimelea vya amiba hasa hasa jamii ya Entamoeba histolytica.

Vimelea hivi huingia moja kwa moja kwenye mwili wa binadamu kwa kupitia mdomoni na kuenda moja kwa moja kwenye njia ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula mpaka kufika kwenye utumbo mkubwa.

DALILI ZA UGONJWA WA AMIBA NI PAMOJA NA;

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi chenye vitu kama makamasi

- Mgonjwa kuanza kupata maumivu ya tumbo sana mithili ya tumbo kusokota

- Mgonjwa kuanza kujisaidia choo kilaini sana

- Mgonjwa kuharisha au kujisaidia haja kubwa ya maji maji sanaa

- Mgonjwa kujisaidia kinyesi ambacho kimechanganyika na damu

- Mgonjwa kutoa hewa kwa njia ya haja kubwa mara kwa mara(kujamba)

- Mgonjwa kupata maumivu ya tumbo,Kifua na viungo mbali mbali vya mwili

- Joto la mwili la mgonjwa kupanda au mgonjwa kuwa na Homa

- Mgonjwa kupatwa na tatizo la kupungukiwa na damu 

- Kupoteza appetite ya chakula kabsa

- Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefu chefu pamoja na kutapika

- Mgonjwa kupungua uzito wa mwili na kukonda

KUMBUKA; Moja ya njia ya mtu kupata vimelea hivi vya amoeba ambavyo husababisha ugonjwa huu wa amiba ni pamoja na kunywa maji machafu sana.

Maji ambayo yamechanganyika ma kinyesi cha mtu ambaye alikuwa na vimelea hivi vya amoeba.

Dalili kuu Nyingine(Summary);

  • Kuharisha mara kwa mara
  • Maumivu ya tumbo
  • Kukakamaa kwa tumbo
  • Kichefuchefu
  • Damu kwenye choo (kwa wagonjwa wachache)
  • Homa katika maambukizi makali

Muhimu: Kuharisha damu, homa kali, au maumivu makali ya tumbo yanaweza kuashiria amiba kali inayohitaji matibabu ya haraka hospitalini.

Takwimu

  • Takribani asilimia 10–20 tu ya walioambukizwa hupata dalili za ugonjwa. Wengi hubaki bila dalili.
  • Utafiti wa kimataifa unaonyesha amiba huathiri mamilioni ya watu duniani na husababisha zaidi ya vifo 55,000 kila mwaka.

Uzoefu wa wagonjwa

Baadhi ya wagonjwa wameripoti:

"Nilikuwa na maumivu ya tumbo na kuharisha kwa muda mrefu hata baada ya matibabu."

Wengine walieleza kuvimbiwa, kujaa gesi tumboni, uchovu na kurudi kwa dalili baada ya muda, jambo linalohitaji uchunguzi wa daktari ili kuthibitisha kama maambukizi bado yapo au kuna tatizo jingine.

Maoni ya madaktari

Madaktari wa Vituo vya kudhibiti na kuzuia Magonjwa "Centers for Disease Control and Prevention(CDC)" wanaeleza kuwa amiba inaweza kutibiwa kwa dawa maalumu za kuua vimelea, lakini uchunguzi sahihi wa kinyesi au vipimo vingine ni muhimu kabla ya matibabu.

NANI YUPO KWENYE HATARI YA KUPATA UGONJWA WA AMOEBA(AMOEBIASIS)

Ingawa mtu yoyote anaweza kuugua Ugonjwa wa amoeba, Tatizo hili huwapata sana watu ambao wanaishi kwenye mazingira machafu,

Lakini Pia baadhi ya Tafiti zinaonyesha Ugonjwa wa Amoeba(amoebiasis) huwapata sana Wanaume wanaoshiriki Mapenzi na wanaume wenzao

MATIBABU YA UGONJWA WA AMIBA

Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu wa amiba

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Kuzuia Ugonjwa wa Amoeba:

Kuzuia ugonjwa wa amoeba ni muhimu sana ili kuepuka madhara ya kiafya. Baadhi ya njia za kuzuia ugonjwa huu ni pamoja na:

✓ Kufuata kanuni zote za usafi wa mazingira

✓ Kunywa maji safi na salama

✓ Kula chakula kilichoandaliwa vizuri

✓ Nawa Mikono kwa Sabuni na Maji safi kabla ya kula au kunywa kitu chochote.

Links data Used;

  • World Health Organization(who)
  • Centers for Disease Control and Prevention(CDC)
  • Cleveland Clinic
  • Médecins Sans Frontières
  • MSF Medical Guidelines:

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584