Head

✍️Author: Dr. Ombeni
🛡️Review: AfyaClass

Tatizo la Mdomo Kuwa Mwekundu: Sababu, Dalili na Tiba

Tatizo la mdomo kuwa mwekundu kupita kiasi linaweza kuwa la muda mfupi au ishara ya ugonjwa unaohitaji matibabu. Uwekundu wa midomo unaweza kuathiri mdomo wa juu, wa chini au pembe za mdomo, na mara nyingi huambatana na ukavu, kuwasha, kuungua au kupasuka.

Takwimu

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO) na wataalamu wa afya ya ngozi, matatizo ya midomo yanayohusiana na ukavu, mzio, maambukizi na upungufu wa virutubisho ni miongoni mwa matatizo yanayoonekana mara kwa mara katika vituo vya afya duniani. Watu wanaoishi kwenye maeneo yenye joto kali, upepo mkali au wanaokosa maji ya kutosha mwilini huwa katika hatari zaidi.

Sababu za Mdomo Kuwa Mwekundu

1. Ukavu wa Midomo (Chapped Lips au dry mouth)

Ukosefu wa maji mwilini, hali ya hewa ya joto au baridi kali unaweza kufanya midomo kuwa mikavu, Myekundu na kupasuka pia.

2. Mzio (Allergic Reaction)

Baadhi ya dawa za meno, vipodozi, lipstick, vyakula au dawa vinaweza kusababisha mdomo kuwa mwekundu kutokana na mzio.

3. Maambukizi ya Fangasi

Fangasi aina ya Candida wanaweza kusababisha wekundu kwenye midomo au pembe za mdomo.

4. Upungufu wa Vitamini

Ukosefu wa vitamini B12, folate na madini ya chuma unaweza kusababisha mabadiliko ya rangi ya midomo na kuifanya iwe nyekundu au kuvimba.

5. Cheilitis

Huu ni uvimbe wa midomo unaoweza kusababishwa na jua kali, maambukizi, mzio au tabia ya kulamba midomo mara kwa mara.

6. Maambukizi ya Virusi

Virusi kama Herpes Simplex vinaweza kusababisha uwekundu, malengelenge na maumivu kwenye midomo.

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO AU LIPS ZAKE KUWA NYEKUNDU SANA

Tatizo la mdomo kwa ndani au kwenye lips kuwa na rangi nyekundu sana kuliko kawaida huweza kutokea kwa mtu yoyote, na kwa wengine hali hii huambatana na maumivu, kuhisi kuchomwa chomwa mdomoni,kuwashwa,kuvimba n.k

Maeneo ambayo huweza kuathirika na tatizo hili la wekundu usio wa kawaida ni pamoja na; mdomo(ndani),lips, ulimi pamoja na Fizi za meno.

CHANZO CHA TATIZO LA MDOMO AU LIPS ZAKE KUWA NYEKUNDU SANA

- Tatizo hili huweza kumpata mtu kutokana na sababu mbali mbali lakini sababu kubwa huweza kuwa mbili yaani;

1. Mtu kupata tatizo la kuumia mdomoni

2. Au kushambuliwa na vimelea vya magonjwa mbali mbali kama vile;

Bacteria,virusi au Fangasi ambao hushambulia ngozi nyembamba ndani mdomoni au kwenye lips

Hivo basi, tunaweza kusema magonjwa ambayo husababisha hali hii ni kama vile;

- Maambukizi ya virusi vya ukimwi

- Maambukizi ya virusi vya Herpes Simplex Virus

- Maambukizi ya Fangasi wa mdomoni

- Maambukizi ya fangasi wa kwenye ulimi n.k

3. Mtu kuwa na Matatizo kama leukemia pamoja na magonjwa mengine kama ya Ngozi,Saratani mdomoni n.k

4. Mtu kuwa na tatizo la Allergies au Mzio kwenye vitu mbali mbali ikiwemo vyakula,nyama,mafuta n.k

5. Upungufu wa Virutubisho mwilini kama Vile Vitamin B n.k, ambapo moja ya dalili zake ni pamoja na;

- Mdomo au Lips za mdomo kubadilika rangi na kuwa nyekundu n.k

- Mdomo kukauka Sana

- Mdomo,Lips za mdomo au Ulimi kupasuka n.k

DALILI AMBAZO MTU MWENYE TATIZO HILI HUWEZA KUZIPATA

• Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

• Mgonjwa kupata uchovu wa mwili usio wa kawaida

• Mdomo wa mgonjwa kukauka sana kuliko kawaida

• Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula

• Mgonjwa kuhisi hali ya kuchomwa chomwa au kuungua moto mdomoni

• Mgonjwa kuanza kupata vipele au vidonda mdomoni

• Na kwa wengine mdomo huanza kuvimba wenyewe

Dalili Zinazoweza Kuambatana Nazo

  • Midomo kuwa nyekundu kupita kawaida
  • Kuwasha au kuungua
  • Kupasuka kwa midomo
  • Kuvimba
  • Maumivu wakati wa kula
  • Kutokwa na ngozi ya midomo

Uzoefu wa Wagonjwa

Wagonjwa wengi huripoti kuwa tatizo huanza kwa ukavu mdogo kisha midomo kuwa nyekundu na kuwasha. Wengine hupata nafuu baada ya kuongeza unywaji wa maji, kutumia mafuta ya midomo au kutibiwa mzio na maambukizi yaliyokuwa chanzo cha tatizo.

Madaktari Wanasemaje?

Madaktari wa ngozi wanashauri kuwa uwekundu wa midomo unaodumu kwa zaidi ya wiki mbili, unaoambatana na maumivu makali, vidonda au uvimbe mkubwa unapaswa kuchunguzwa hospitalini ili kubaini chanzo halisi.

MATIBABU YA TATIZO HILI

- Mgonjwa ataanza kupata matibabu kulingana na chanzo chake, mfano kama ni maambukizi ya fangasi wa mdomoni, mgonjwa ataanza kutibiwa fangasi, Kama ni maambukizi ya bacteria basi tiba itahusu eneo hili n.k

Tiba

Tiba hutegemea chanzo:

  • Kunywa maji ya kutosha
  • Kutumia mafuta ya midomo (lip balm)
  • Kuepuka vitu vinavyosababisha mzio
  • Kutibu fangasi au maambukizi kwa ushauri wa daktari
  • Kutumia virutubisho iwapo kuna upungufu wa vitamini au madini

Wakati wa Kumwona Daktari

Muone daktari ikiwa:

  • Midomo imekuwa myekundu kwa muda mrefu
  • Kuna vidonda visivyopona
  • Kuna uvimbe mkubwa
  • Unapata homa au maumivu makali
  • Tatizo linajirudia mara kwa mara

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Vyanzo Vilivyotumika (Links Used)

#Reply

#5Replies
🔥 CHAT NASI
Dr. Ombeni Dr. Ombeni
Je, una changamoto yoyote ya Kiafya? Kwa Ushauri & Tiba tuwasiliane. Call (Kawaida) au SMS (WhatsApp): +255 758 286 584